
Muonekano wa sehemu ya lori lililohusika kwenye ajali, Simiyu
Kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu, ACP Blasius Chatanda amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwataja watu waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni Joseph Nsungi Sasa (31) Mkazi wa Bunamala, Lameck Sayi Lyaganda, (32) mkazi wa ibulyu, Pagi Hima Peme, (16)mkazi wa Ibulyu, Joseph Nzumbi (22) mkazi wa Kidalimanda, Shinda Maige Hima, (17) mkazi wa Ibulyu, Susa Sayi (18) mkazi wa Ibulyu, Masunga Dotto Mbilibili, (32) ambaye ni dereva wa Bajaji.
Kamanda Chatanda amesema kuwa miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia Maiti na Majeruhi Wanaendelea kutibiwa katika Hospitali ya Mji ya Bariadi.
Imetajwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi uliopelekea dereva wa lori kushindwa kulimudu kisha akaigonga Bajaji ambayo iliwaka moto baada ya ajali. Ameongeza kwamba baada ya ajli hiyo derava wa gari hilo alitokomea kusikojulikana na kwamba jitihada za kumtafuta zinaendelea.