
Navas na mkewe Andrea Salas wamejitolea mpaka kununua nguo mpya kwa wakimbizi hao.
Navas na mkewe wamenunua vitanda 30 na kuweka katika chumba cha sinema ndani ya nyumba yao kwa ajili ya wakimbizi hao kupata hifadhi, na mkewe amejitolea kuwaandalia chakula kila siku.
Pia Andrea mke wa Navas ametumia ukurasa wake wa instagram kuwaomba watu watoe msaada kwa raia wa Ukraine ambao wameathiriwa na vita dhidi ya Urusi katika ardhi yao ya nyumbani.