Saturday , 19th Feb , 2022

Ni headlines za msanii Dogo Janja zikimuonyesha akiwa mapumzikoni na kufanya utalii akiwa na Simba ambao amewashika mkia.

Picha ya Dogo Janja akiwa na Simba

Dogo Janja ameshea picha akiwa na simba hao kwenye Instagram yake na kuandika kuchunga Simba ni raha sana, na Simba ni mnyama ni rafiki mwema kuliko binaadam.

Aidha kwenye post yake nyingine akiwaelezea Simba hao Janjaro anasema "Ukiwa muoga na kusita sita, anaweza akakubadilikia muda wote na kukufanya chochote anachotaka, kiufupi kama hauna ujasiri hii sio ya kujaribu kaa nyumbani mshike tu paka wako hawa tuachie sisi".