
Lionel Messi akiwa katika jezi ya Barcelona.
Mshindi huyo mara sita wa Ballon d'Or ambaye alikuwa na machaguo mengine mawili kabla ya kuamua kujiunga na PSG ambayo itamlipa mshahara wa euro Milioni 25 kwa mwaka baada ta kodi.
Messi mwenye umri wa miaka 34, alikubali kusalia Barcelona kwa mkataba wa miaka mitano ambao ungemfanya apokee nusu ya mshahara wake wa awali lakini kutokana na ukata wa fedha na vikwazo vya kikanuni nyota huyo anaondoka kama mchezaji huru.
Mashabiki wa klabu ya PSG wamefurika katika viunga vya klabu hiyo wakisubiria kumuona mchezaji huyo bora kuwahi kutokea Duniani katika miaka 25 iliyopita.