Tuesday , 3rd Aug , 2021

Klabu ya Yanga imemtambulisha mshambuliaji Heritier Makambo raia wa Kongo, mshambuliaji huyo anarejea Yanga baada ya misimu miwili tangu auzwe kwenda katika klabu ya Horoya AC ya Guinea na amesaini mkabata wa miaka miwili.

Makambo anakuwa mchezaji wa tatu kutambulisha katika klabu ya Yanga baada ya hapo awali klabu hiyo kuwatambulisha wachezaji Fiston Mayele na Yusuph Athumani ambao wote hawa ni washambuliaji.

Heritier anarejea akiwa mchezaji huru baada ya kuachana na klabu ya Horoya, na anarejea kwenye kikosi cha wananchi kwa mara ya pili baada ya kukitumikia kikosi hicho msimu wa 2018-19, ambapo msimu huo alifunga jumla ya mabao 21 kwenye michezo 40 kwenye michuano yote huku mabao 17 kati ya hayo ni ya Ligi Kuu Tanzania bara.