Tuesday , 3rd Aug , 2021

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Elias John Kwandikwa amefariki dunia, usiku wa Agosti 2, 2021.

Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Elias John Kwandikwa enzi za uhai wake

Kwa mujibu wa Msemaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminieli Eligaesha amesema kuwa Waziri Kwandikwa alikuwa akipatiwa matibabu hospitalini hapo kwa takribani wiki mbili.

''Marehemu Elias Kwandikwa alikuwa amelazwa hapa kwetu kwa takribani siku 14 na majira ya saa 2:20 usiku siku ya jana Agosti 2, 2021 akafariki dunia," ameeleza Aminieli Eligaesha.