Monday , 2nd Aug , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amewambia wananchi wa  Rwanda kuwa Tanzania kuna utulivu wa kutosha na ipo salama.

Kushoto ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame

Kauli hiyo ameitoa hii leo Agosti 2, 2021, nchini Rwanda, wakati akizungumza mbele ya Rais wa Rwanda Paul Kagame, ikiwa ni ziara yake ya siku mbili kufuatia mwaliko wa Rais wa nchi hiyo.

"Nataka niwaambie Tanzania tupo na utulivu na usalama wa kutosha, kwa kiasi kikubwa mazungumzo yetu yalijikita katika kuimarisha, kukuza ushirikiano wa kiuchumi kati yetu kama mnavyojua kwenye Dunia ya sasa uhusiano baina ya Mataifa umejikita zaidi katika masuala ya kiuchumi," amesema Rais Samia

Kuhusu mashirikiano kati ya nchi hizo mbili, Rais Samia amesema, "Leo tumesaini makubaliano kwamba tunaendeleza mahusiano mazuri kwenye matumizi ya TEHAMA, niwapongeze Rwanda mpo mbele yetu na sisi tupo tayari kuja kujifunza kwenu, pia kwenye masuala ya COVID-19  tumeweka mkakati wa kushirikiana, tumekubaliana kuendeleza ushirikiano uliopo"