Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu
Waziri Ummy amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari leo, wakati akitoa taarifa za makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri ambapo ametaka fedha zikikusanywa kupeleka benki ndo zitumike.
"Nielekeze Halmashauri kuhakikisha fedha za makusanyo ya ndani zinazokusanywa zinapelekwa benki ndani ya masaa 24 baada ya kuzikusanya ni marufuku na kosa kisheria kwa halmashauri kutumia fedha zilizokusanywa kabla ya kuzipeleka benki (Fedha mbichi) ” amesema Waziri UMMY
"Wakuu wa idara na wakurugenzi ni marufuku kuchukua fedha mbichi amabazo zimekusanywa na hazijapelekwa benki hata kama kuna dharura yeyote , fedha zipelekwe benki ndo zitumike, benki unaweka hela na unatoa siku hiyohiyo” alisisitiza Waziri Ummy
Aidha Waziri Ummy amezitika Halmashauri zote nchini kukamilisha miradi ya maendeleo kwa kutumia fedha za ndani badala ya kusubiria fedha kutoka serikali kuu.
“Nitaishangaa halmashauri ambayo itashindwa kujenga hata nyumba moja ya mwalimu kwa mwaka kwasababu tumepeleka walimu vijijini changamoto kuu ni nyumba za walimu, nataka halamashauri sasa hivi nazo zijenge nyumba za walimu na taarifa zetu inaonyesha mil 50 unajenga nyumba ya kuweka kaya mbili za walimu,” amesema Mhe. Ummy
Waziri Ummy ametoa taraifa ya makusanyo nakuzitaja Halmashauri zilizongoza kwa kukusanya mapato mengi kuwa ni Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam sh. Bil.67.09 , ikifuatiwa na Manispaa ya Kinondoni Bil 40.7 na Halmashauri ya Dodoma Bil.38.4 huku Halmashauri 9 zikiwa zimekusanya chini ya Bil 1.