Wednesday , 28th Jul , 2021

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk. Faustine Ndugulile, amesema kuwa serikali itaanza kuzima laini zote ambazo hazijahakikiwa kwani hadi sasa watu zaidi ya milioni 10 wanaomiliki laini za simu ambazo hazijahakikiwa.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk. Faustine Ndugulile

Dk. Ndugulile ameyasema hayo leo Jijini Dodoma ambapo amebainisha kuwa kwa kipindi cha robo mwaka yaani kuanzia Aprili hadi Juni laini elfu 18, 622 zimefungiwa kutokana na kufanya vitendo vya kihalifu kwa njia ya mtandao.

Dk. Ndugulile ameongeza kwa kusema kuwa vitambulisho vilivyotumika kusajilia laini elfu 14,768 vimezuiliwa baada ya kuonekana vinatumika na matapeli na hatua inayofuatia ni kuwafungulia mashtaka Mahakamani wahusika ili kukabiliana na wimbi la utapeli wa mtandaoni.