Tuesday , 27th Jul , 2021

Big Cat wa BongoFlava Bonge la Nyau 'Nyauloso' amesema watu wa aina yake mashombeshombe huwa wanasumbuliwa na wanawake kwa kuwataka kuwa nao kwenye mahusiano.

Picha ya msanii Bonge la Nyau

Bonge la Nyau ametoa kauli hiyo wakati akijibu  madai ya stori zinazosemekana kwamba Producer wake Bob Junior amepotea kwenye game kwa sababu ya kuponzwa na wanawake na stress.

"Stress kila binadam anazo kuhusu wanawake sidhani, Bob Junior ni shombeshombe kama mimi na si unajua mashombeshombe tunasumbuliwa na wanawake, sioni kama wanawake wanaweza kumfanya akae kimya kwenye muziki yeye sio mgeni wa wanawake" amesema Bonge la Nyau

Mengine zaidi akimzungumzia Bonge la Nyau tazama hapo chini kwenye video.