Thursday , 1st Jul , 2021

'SPORT COUNTDOWN' ya East Africa redio ya leo Julai 1,2021. Ni dondoo za michezo zinazokujia lika siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa moja na robo kutoka kipindi cha Super breakfast kutoka kwa wachambuzi wako Ibrahim Kasuga 'Mtaalam wa soka' na Abissay Stephen Jr.

Nyota wa Scotland, Andy Murray akiwa mchezoni dhidi ya Oscar Otte kwenye mchezo wa mzunguko wa pili wa tenisi Wmbledon usiku wa kuamkia leo.

6 – Ni idadi ya michezo iliyochgezwa kwenye fainali ya ligi ya kikapu nchini Marekani 'NBA' kwa ukanda wa Magharibi na kushuhudia timu ya Pheonix Suns ikiibuka mabingwa baada ya alfajiri ya kuamkia leo kuifunga timu ya Los Angeles Clippers kwa alama 130-103 na kushinda michezo 4-2 na kuweka rekodi ya kutinga fainali ya NBA inayokutanisha mabingwa wa kanda zote kwa mara ya kwanza toke mwaka 1993.

Nyota wa Suns, Chris Paul ndiye aliyeibuka kuwa shujaa wa mchezo huo baada ya kufikisha alama 41, rebaundi 4 na assisti 8, assisti 8 alizotoa zimemfanya mkali huyo kufikisha assisti 1,022 tokea aanze kukipiga kwenye NBA na kushika nafasi ya 11 kwenye orodha ya muda wote ya NBA kwa wachezaji wenye assisti nyingi na kubakisha assisti 17 kumfikia gwiji Kobe Bryant anayeshika nafasi ya 10 akiwa na assisti 1,040.

NBA itaendelea tena alfajiri ya kuamkia kesho kwa mhezo mmoja wa mzunguko wa 5 wa fainali ya ukanda wa mashariki ambapo Milwaukee Bucks itakipiga na Atlanta Hawks saa 9:30 kumkia Julai 2 huku wawili hao wakiwa wametoshana nguvu ya kushinda michezo 2-2.

5 – Ni idadi ya makocha waliohusishwa kujiunga na timu ya Tottenham Hotspurs 'Masharobalo wa jiji la London' lakini hatimaye kocha wa zamani wa Wolves, Nuno Espirito Santo amefanikiwa kuwapiku wenzake na kuibuka kuwa kocha mpya wa Spurs na kusaini kandarasi ya miaka miwili .

Makopcha waliohusishwa kujiunga na Spurs ni Antonio Conte, Mauricio Pochettino, Paul Fonseca, Gennaro Gattuso na Julen Lupotegui.

4 – Idadi ya michezo ya hatua ya robo fainali ya michuano ya UEFA EUROS itakayochezwa hivi karibuni, lakini miwili itakayochezwa kesho Julai 2, ni ule utakaowakutanisha Uswizi iliyotinga hatua hiyo kwa mara ya kwanza tokae 1954 dhidi ya Bingwa wa kihistoria, Hispania saa 1:00 usiku wakati Ubelgiji itacheza dhidi ya Italia saa 4:00 usiku huenda bila ya wachezaji wake nyota Kevin Debruyne na Eden Hazard kutokana na majeraha wakati Julai 3, timu ya Jamhuri ya Czech itacheza dhidi ya Denmark saa 1:00 usiku ilhali Ukraine iliyofuzu pia kwa mara ya kwanza itacheza na timu ya malkia England saa 4:00 usiku.

3 – Ni tarehe ambayo bingwa mtetezi wa COPA AMERICA ya Amerika Kusini, timu ya taifa ya Brazil itashuka dimbani ikiwa ni siku ya kesho Julai 3 kwenye robo fainali ya michuano hiyo huku timu ya PERU wakitaraji kucheza na Paraguay saa 6:00 usiku na kuendelea tena siku ya Jumapili Julai 4 mwaka huu, bingwa wa kihistoria timu ya Uruguay dhidi ya Colombia saa 7:00 usiku na aliyekuwa kinara wa kundi A, Argentina itachuana na Ecuardo saa 10:00 Alfajiri.

2 – Idadi ya siku zilizosalia kuelekea derby ya kariakoo siku ya Jumamosi, Julai 3 mwaka huu, na kuelekea kwenye mchezo huo, klabu ya Yanga imethibitisha kurejea kikosini kwa beki wake kitasa Abdallah Shaibu almaarufu 'Ninja' aliyekuwa nje ya dimba takribani miezi miwili kutokana na majeraha ilhali Simba kupitia Afisa Msemaji wake, Haji Manara imesema haina wachezaji wenye majeraha mapya. 

Mchezo huo utakaochezwa saa 11:00 jioni utatangazwa mubashara na East Africa Redio kutoka dimba la Benjamin William Mkapa.

1 – Ni nafasi ya ubora ya mcheza tenisi Andy Murray anayoishikilia nchini kwao Scotland lakini ni wa 118 kwenye viwango vya tenisi Duniani na usiku wa kuamkia leo alishuka dimbani kucheza dhidi ya Oscar Otte raia wa Ujerumani mwenye umri wa maiaka 22 na anayeshika nafasi ya 151 kwenye viwango vya bora na kumfunga kwa seti 6-3, 4-6, 4-6 na 6-2 na kufanikiwa kutinga hatua ya mzunguko watatu wa michuano hiyo ya Wimbledon.

Murray mwenye miaka 34 sasa atacheza dhidi ya Mkanada mwenye miaka 22, Denis Shapovalov anayeshika nafasi ya 10 kwa ubora Duniani siku ya kesho Ijumaa Julai 2 kwenye mchezo wa mzunguko watatu wa Wimbledon.