Wednesday , 30th Jun , 2021

Timu ya taifa ya Ukraine imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya UEFA EUROS ikiwa ni kwa mara ya kwanza baada ya kuifunga Sweden mabao 2-1 kwenye mchezo ulioamuliwa na dakika 30 za nyongeza kufuatia sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za mchezo.

Mshambuliaji wa Ukraine, Marcus Danielson akishangilia bao la ushindi la kuivush atimu yake kucheza robo fainali ya kihistoria ambapo watacheza na England.

Mabao ya Ukraine yamefungwa na Oleksandra Zinchenko dakika ya 27', Emile Forsburg aliishawazishia Sweden. Shujaa wa mchezo huo alikuwa ni Marcus Danielson aliyepachika bao la ushindi dakika ya moja ya niongeza baada ya 30 kukamilika.

Ukraine imetinga hatua hiyo kwa mara ya kwanza na kocha mkuu wa timu hiyo, mshambuliaji wa zamani wa AC Milan ya Italia, Chelsea ya England na Dynamo Kiev ya nchini Ukraine, Andry Shevchenko amabye aliiongoza timu hiyo kucheza hatua ya robo fainali ya kombe la Dunia kwa mara ya kwanza 2006 akiwa nahodha.

Ukraine sasa itacheza na timu ya Taifa ya England Julai 2, 2021 saa 4:00 usiku, Jamhuri ya Czech itapapatuana na Denmark saa 1:00 usiku siku hiyo hiyo ilhali Uswizi na Hispania watacheza saa 1:00 usiku Julai 3 wakati ambao Ubelgiji watacheza dhidi ya Italia saa 4:00 usiku.