Wednesday , 30th Jun , 2021

Timu ya Atlanta Hawks imefanikiwa kuibuka na ushindi wa alama 116-88 dhidi ya timu ya Milwaukee Bucks kwenye mchezo wa mzunguko wa nne wa fainali ya ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani 'NBA' kwa ukanda wa Mashariki.

Nyota wa Atlanta, Lou Williams akijaribu kutaka kwapita walinzi wa Milwaukee Bucks, Khris Middletone (kushoto) na Anthony Leon 'P.J Tucker' (kulia) kwenye mchezo wa Alfajiri ya kuamkia leo.

Atlanta ilikuwa inaongozwa kwenye michezo miwili iliyopita wakiwa na ushindi mmoja, jambo lililowafanya kupamabana na kuonesha kiwango safi mbele ya Bucks bila hata ya nyota wake Trae Young kutokuwepo kutokana na majeraha ya mguu yaliyoanza kumsumbua tokea mchezo uliopita.

Nafasi ya Young ilizibwa vizuri na Lou Williams ambaye alifikisha alama 21, rebaundi 5 na assisti 8 na kuibukla kuwa mchezaji nyota wa mchezo huo na kumpiku Giannis Antetokounmpo wa Bucks ambaye aliishia kucheza dakika 24 pekee na kutoka kutokana na majeraha ya mguu.

Kwa matokeo hayo, wawili hao wametoka sare baada ya kila timu kuwa ushindi wa michezo miwili  hivyo mbio za kuwania kombe la NBA kwa ukanda huo limeamka upayaaa!.

Mchezo wa fainali nyingine ya NBA kwa ukanda wa Magharibi kati ya Los Angeles Clipppers dhidi ya Phoenix Suns inataraji kuchezwa saa 10:00 Alfajiri wa kuamkia kesho Julai mosi huku Suns akihitaji ushindi pekee ili kutangazwa kuwa mabingwa waukanda huo.