Wednesday , 30th Jun , 2021

Mcheza tenisi anayeshika nafasi ya nane kwenye viwango vya ubora Duniani kwa mujibu wa Chama cha wacheza tenisi cha Wanawake Duniani, Serena Williams ameshindwa kuendelea na mchezo wake katika michuano ya Wimbledon usiku wa kuamkia leo baada ya kupata maumivu ya mguu.

Serena Williams akiangulia kilio baada ya kupata maumivu ya misuli kwenye mguu wake wa kulia na kushindwa kuendelea na mchezo wa mzunguko wa pili kwenye michuano ya Tenisi ya Wimbledon.

Serena ambaye ni wa Marekani alikuwa dimbani kwenye mchezo wa mzunguko wa  pili dhidi ya Aliaksandra Sasnovich wa Belarus na kufukuzana kwenye seti ya tatu wakiwa na alama 3-3 lakini nyota huyo alishindwa kuendelea na mchezo huo baada ya maumivu ya misuli ya paja lake la kulia.

Serena anayetaraji kutimiza miaka 40 mwezi Septemba mwaka huu, aliugulia maumivu hayo yaliyomlekea kujiinamia chini na kuanza kutokwa na machozi na kuonesha kushindwa kuendelea na mchezo huo jambo ambalo lilipelekea apigiwe makofi ya heshima na mashabiki ili kumfariji.

Baada ya kupatiwa matibabu ya awali na kurejea kambini, Serena aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa “Niliumia sana kuondoshwa baada ya kupata maumivu kwenye mguu wangu wa kulia”.

“Upendo na shukrani zangu zipo na mashabiki na wote waliofanya nipate faraja uwanjani. Nimepata hisia kubwa sana kuungwa mkono na umati wa mashabiki wakati natolewa uwanjani na wao wanaana kubwa sana kwangu”.

Kilichomkuta Serena Willians ni huzuni kwani alikuwa anasaka ushindi wa 24 wa michuano hiyo mikubwa ya Tenis ili kuweka rekodi ya kipekee kuwa mwanadada pekee kutwaa mataji mengi zaidi kwenye historia ya tenisi huku wengi wakisema huenda ni michuano yake ya mwisho kutoka na umri wake kuwa mkubwa na majeraha yanayomuandama.

Baadhi ya wacheza tenisi nyota kama Vile Andy Murray kwa upande wa wanaume na mwanamama Tracy Austin ambaye ni gwiji wa zamani wa mchezo huo kwenye miaka ya 1980 aliyewahi kushika nafasi ya kwanza kwa ubora duniani pamoja na kushinda Gland Slam 3.