Monday , 14th Jun , 2021

Producer aliyetengeneza mdundo wa Ndombolo ya Kings Music Records Swabri Made it, amesema idea ya lebo hiyo imetoka kwa msanii wake K2ga ambaye ndio alikuwa wa kwanza kufika studio na kurekodi.

Kushoto ni picha ya Producer Swabri Madeit kulia ni msanii K2ga

"Ngoma ya Ndombolo wakati natengeneza beat alikuja K2ga studio, akawa anaandika kisha akarekodi kipande kisha akaomba aondoke nayo, alivyofika akawasikilizisha ile chorus wakaipenda, kesho yake asubuhi wakanipigia simu niende studio kwao Tabata" amesema Swabri Made it

"Idea ilikuwa ya K2ga ndio maana alikuwa wa kwanza kuimba kwenye Ndombolo, studio kulikuwa na mizuka sana na Alikiba alikuwa hataki kuimba kwa sababu ana verse nyingi" ameongeza

Ndombolo ni ngoma ya kwanza ya Kings Music Records baada ya ukimya wa miaka miwili bila kutoa wimbo wowote kama lebo, pia inafanya vizuri kwa sasa mitandaoni kutokana na Challenge ya Alikiba na mtoto wake wanavyocheza.