Wednesday , 2nd Jun , 2021

Mchekeshaji Anko Zumo ametoa kali ya mwaka kwa kusema mara yake ya kwanza kupigwa busu na mwanamke alitaka kuzimia kwa sababu alikuwa hajazoeshwa mambo hayo. 

Mchekeshaji Anko Zumo

Anko Zumo amefunguka hilo kwenye show ya DADAZ ya East Africa TV ambapo wamezungumzia suala la wazazi wa kiume kuwa karibu na watoto wao wa kike kama kumkumbatia na kum'busu kitendo ambacho kinatafsiriwa tofauti kwa baadhi ya watu kwenye jamii.

"Busu likitoka kwa Baba kwenda kwa mtoto wake wa kike akikua mtu mzima anakuwa sio mlimbukeni tena wa busu, mimi mara yangu ya kwanza kupigwa busu ilikuwa bado kidogo nizimie kwa sababu nilikuwa sijazoeshwa mambo hayo lakini sasa hivi nimeshazoea" amesema Anko Zumo