Friday , 28th May , 2021

Sherehe za utoaji wa Tuzo za Oscars za msimu wa 94 zilizokuwa zimepangwa kufanyika mwezi Februari 27, 2022 zimesogezwa tena mbele mwezi mmoja, na sasa zitafanyika Machi 27, 2022 sababu ikielezwa kuwa ni janga la Virusi vya Corona.

The Academy Awards

Hii sasa itakuwa ni mara ya pili mfululizo kwa Tuzo hizo za Oscars kuahirishwa, na ratiba mpya imetoka ya matukio yote yaliyopangwa kufanyika kwenye ukumbi wa Dolby Theatre huko Hollywood & Highland Center ambapo kwasasa ukumbi huo  umefungwa kutokana na janga hilo.

Picha ya Tuzo za Oscars

The Academy Awards (Oscars) Hufanyika kila mwaka na kampuni ya Academy of Motion Picture Arts and Sciences (AMPAS) kwa lengo la kutambua mchango wa taaluma ya tasnia ya filamu, wakiwemo waongozaji, waigizaji, na watunzi wa filamu.