Monday , 24th May , 2021

Vigezo na masharti vizingatiwe pale mtu anapochagua kitu anachokipenda, msanii Marioo  amesema akimtaka mwanamke wa kuingia kwenye mahusiano basi huangalia umbo kwanza, kisha mengine baadae.

Picha ya msanii Marioo

Kupitia EATV & EA Radio Digital, Marioo amesema kwa sasa yupo 'single' ila anataka kuwa na mwanamke ambaye hata akifika mahali watu waogope kutokana na muonekano wake.

"Vigezo na masharti vizingatiwe, kwanza lazima awe mtoto mzuri na mkali nikitokea naye sehemu fulani watu wanaogopa, sio unatembea na mwanamke watu hata hawamuangalii, mimi kwanza napenda umbo na jinsi alivyo kama tabia zake nitajua baadae" amesema Marioo