Monday , 24th May , 2021

Mbunge wa Mtama Mhe. Nape Nnauye, ameishauri serikali kupitia Wizara Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na TANPA kuhakikisha wanalima zao la pilipili pembezoni mwa vijiji vinavyopakana na hifadhi ili kuwanausuru wananchi kuuliwa na tembo pamoja na mazao yao kuharibia na wanyama hao.

Mbunge wa Mtama Mhe. Nape Nnauye

Kauli hiyo Mhe. Nnauye ameitoa leo Bungeni Jijini Dodoma, wakati akiuliza swali la nyongeza kwa Wizara ya Maliasili na Utalii.

"Wizara imekuwa ikisema kwamba upandaji wa pilipili kwenye maeneo ya vijiji ambayo yanakaribiana na hifadhi kuna uwezo wa kuzuia tembo kuingia vijijini, Je, serikali ipo tayari kupitia TANAPA na taasisi zake wakapanda wao hizo pilipili ili kuwasaidia wananchi wetu mazao yao yasiliwe na wao wasiuliwe?," aliuliza Mhe. Nnauye.