
Pichani muonekano wa Soko la Kariakoo, Jijini Dar es Salaam.
RC Kunenge amesema Serikali inatambua na kuthamini Mchango wa wamachinga kwenye Mkoa huo hivyo amewataka waendelee kufanya biashara zao kwa kufuata Sheria, kanuni na taratibu.
Aidha RC Kunenge amewataka wamachinga wasijenge kwenye mapito ya watembea kwa miguu wala barabarani kwani kwa kufanya hivyo wanahatarisha usalama wao na vyombo vya moto.
Pamoja na hayo RC Kunenge ametoa angalizo kwa Wafanyabiashara wenye utaratibu wa kubeba mitungi ya gesi na majiko yanayowaka na kukatizanayo katikati ya watu na Vyombo vya Moto Jambo ambalo ni hatari kwa kiusamama.