Saturday , 1st May , 2021

Nyota wa timu ya Washington Wizard, Russell Westbrook ameibuka na alama 15, rebaundi 12 na assisti 11 kwenye mchezo wa usiku wa kuamkia leo dhidi ya Cleveland Cavaliers kwenye Ligi kuu ya kikapu Marekani na kufikisha jumla ya ‘Triple-double’ yake ya 31 msimu huu.

Russell Westbrook akimpita mlinzi wa timu ya Denver Nuggets kwenye mchezo wa NBA wa mzunguko wa pili.

Westbrook sasa amefikisha jumla ya ‘Triple-double’ 177 tokea aanze kukipiga kwenye NBA mwaka 2008 na kufukuzia rekodi ya kufikisha ‘Triple-double’ 181 inayoshikiliwa na Oscar Robertson kwenye historia ya NBA tokea ‘Triple-dpouble’ zilipoanza kuhesabiwa mwaka 1951.

Nyota huyo aliye kwenye kiwango bora kwa sasa amebakisha michezo 9 kuifukuzia rekodi hiyo wakati ambao NBA inakaribia kumaliza mzunguko wa pili wakiwa kwenye nafasi ya 10 kwa upande wa Magharibi kabla ya kuelekea kwenye michezo ya ‘NBA Play-in’ Mei 18, 2021.

Rekodi nyingine zilizowekwa na Westbrook msimu huu, ni pamoja na kukamilisha kuzifunga 'Triple-double' timu zote 30 za NBA pamoja na kupiga 'Multi-Triple-double' nyingi za zaidi ya alama 30, rebaundi 10 na assiti 10.