
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Viwango TBS Dkt Athumani Ngenya
Akizindua Mfumo huo Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Viwango TBS Dkt Athumani Ngenya sambamba na Mkurugenzi wa Trade mark East Africa John Ulanga wameeleza kuwa Mfumo huo utapunguza muda na gharama kwa wadau na wateja kulazimika kufika ofisi za TBS kupata huduma zinazolazimika na udhibiti wa ubora,v iwango uchukuaji wa vibali na vyeti.
"Zamani wadau ilikuwa ikiwalazimu kusafiri umbali mrefu kuchapisha nyaraka ama kuwasilisha. Maombi kwenye makaratasi mchakato ambao ulitawaliwa na makosa na ucheleweshaji," amesema Dkt Athumani.
Aidha amesema ni wakati muhimu sasa kwa wadau hususani wazalishaji waingizaji wa bidhaa mbali mbali kutumia Mfumo huu Ili kurahisisha utendaji kuelekea kasi ya Tanzania ya Viwanda yenye uchumi wa Kati wa juu.
"Utoaji wa huduma za kidijitali umepungiza gharama na muda wa kufanya biashara hivyo kurahisisha ufikiwaji wa malengo ya ukuzaji Viwanda na maendeleo ya uchumi nchni Tanzania" amesema Dkt Athumani