Wednesday , 28th Apr , 2021

Mshambuliaji wa klabu ya PSG ya Ufaransa Neymar Jr ameionya klabu ya Manchester City kuwa atafanya lolote kuhakikisha timu yake inaibuka na ushindi kwenye mchezo wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya utakao zikutanisha timu hizo leo Usiku katika dimba la Parc des Princes.

Neymar da Silva Santos Júnior

Neymar raia wa Brazil ambaye ni mshindi mara moja wa taji la Ligi ya mabingwa ulaya ambalo alishinda mwaka 2015 akiwa na kikosi cha FC Barcelona ya Hispania amesema malengo yake kwa sasa ni kutwaa ubingwa wa michuano hii kwa mara nyingine tena,

“Tutafanya kila kitu kwa uwezo wetu kushinda dhidi ya Manchester City. Nitafanya kila kitu, nikizungumza kwa weledi kushinda mchezo huu. Lengo langu kuu ni Ligi ya Mabingwa na sio kushinda Ballon d'Or, hicho sio kipaumbele changu kwa sasa. Katika siku za usoni ninahitaji kukumbuka kuwa nimeshinda Ligi ya Mabingwa mara moja, mara mbili au labda mara tatu." amesema Neymar

Lakini pia kuelekea mchezo huu kocha wa PSG Mauricio Pochettino amesema ni wachezaji wawili tu ndio watakao kusekana kwenye mchezo huu ambao ni beki wa kushoto Juan Bernat na golikipa wa akiba Alexandre Letellier. Hivyo mshambuliaji Kylian Mbappe ambaye alipata maumivu kwenye mchezo wa ligi mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Metz yupo fiti kucheza mchezo wa leo.

kwa upande wa kocha wa Manchester City Pep Guardiola hana mchezaji hata mmoja mwenye majeruhi, hivyo anauwanda mpana wa kuchagua ni wachezaji gani atawapa nafasi ya kuwa sehemu ya mchezo wa leo usiku.