Wednesday , 28th Apr , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiwa na wajumbe wengine, ameshiriki kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma leo Jumatano Aprili 28, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiwa na wajumbe wengine

Kikao hicho kimeongozwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho (bara) Ndugu Philip Mangula akisaidiana na Makamu wa Mwenyekiti mwenza (Visiwani) Rais Mstaafu wa Zanzibar Ali Mohamed Shein.

Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni sehemu ya vikao vya utangulizi kabla ya Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa ambao utafanyika Aprili 30, 2021 jijini Dodoma.