Friday , 21st Nov , 2014

Serikali imetoa tamko kuhusiana na malalamiko ya Vyama vya siasa kuhusu kuingilia mamlaka ya vyama ya kuwapangia watu wa kuwadhamini Wanachama wao pamoja na Mihuri ambayo inatakiwa kutumika.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda.

Akitoka Kauli ya Serikali jana Bungeni Mjini Dodoma Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda amesema Ofisi yake itatoa maelekezo kwa watendaji hao ili wananchama hao waweze kudhamini kutoka mashina au vitongoji vyao tofauti na ilivyokua awali.

Mh. Pinda ameongeza kuwa hatua ya Kufanya hivyo ni kutokana na migogoro iliyopo sasa ambayo inaonekana itaweza kuwanyima fursa wanachama wengine kushiriki katika chaguzi hizo na kusema hilo ni tatizo ambalo linarekebisha na wamefanya hivyo kwa maslahi ya Vyama vyote.

Aidha Mh. Pinda amewagiza wakurugenzi wote wanaosimamia zoezi la Uchaguzi wa Serikali za mitaa kuhakikisha uandikishwaji unafanyaika kwa kufuata sheria ili kuepuka migongano iliyopo sasa.