Thursday , 20th Nov , 2014

Ligi ya Mpira wa kikapu ya mkoa wa Dar es salaam BD imemaliza mzunguko wake wa kwanza wiki hii ambapo inatarajia kutumia mapumziko hayo kwa ajili ya kumalizia michezo ambayo iliahirishwa katikati ya Ligi hiyo.

Akizungumza na East Africa Radio, Makamu wa Rais wa BD, Richard Julles amesema katika mapumziko hayo kuna baadhi ya vilabu vitakuwa mkoani Dodoma kwa ajili ya kushiriki michuano ya Taifa ya mpira wa kikapu yanayotarajiwa kuanza Desemba mwaka huu.

Julles amesema katika mzunguko wa kwanza wa Ligi kulikuwa na changamoto mbalimbali lakini watajitahidi kuyafanyia marekebisho ili mzunguko wa pili iweze kuwa na ushindani zaidi.