Sunday , 16th Nov , 2014

Timu ya wanawake ya mpira wa magongo inatarajiwa kuondoka nchini kuelekea nchini Zimbambwe kwa ajili ya kushiriki miachuano ya Klabu Bingwa Afrika inayotarajiwa kuanza Novemba 22 mpaka 30 nchini humo.

Akizungumza na East Africa Radio, Makamu mwenyekiti wa chama cha mpira wa Magongo nchini THA,Mnonda Magani amesema michuano hiyo inashirikisha nchi 10 ambapo timu inatarajia kuondoka na wachezaji 15 na kiongozi mmoja.

Magani amesema Tanzania imekuwa moja ya nchi Shiriki katika michuano hiyo kutokana na kutokuwa na timu nyingine Pinzani ambayo inaweza kushiriki michuano hiyo yenye changamoto mbalimbali.