Tuesday , 29th Dec , 2020

Viongozi mbalimbali wa kitaifa wakiongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa, wameungana na waombolezaji wengine kuanga mwili wa aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Mngereza.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa (katikati) akiwa na viongozi wengine.

Zoezi hilo linafanyika leo Disemba 29, 2020, katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es salaam. Mbali na viongozi lakini wasanii na makundi mbalimbali ya sanaa wamefika kumuaga.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza alifariki dunia usiku huu wa Disemba 24, 2020, akiwa hospitali jijini Dodoma.

Waziri wa zamani wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe

Viongozi mbalimbali wa kitaifa, akiwemo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole.