RC Mtwara Gelasius Byakanwa, RC Kagera Brigedia Jeneral Marco Gaguti na timu ya madereva wa bodaboda kutoka mikoa hiyo miwili wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Katika ziara hiyo leo, wakuu hao wa mikoa na waendesha Bodaboda wametembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR na jengo la abiria la Tanzanite, mradi wa mabasi ya mwendo kasi, ujenzi wa stand mpya ya mabasi ya Mbezi Luis, daraja la juu la Ubungo na mradi wa kufua umeme wa Kinyerezi two ambayo ipo chini ya serikali ya Rais Dkt.John Magufuli.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo wa Mkuu wa mkoa Mtwara Gelasius Byakanwa amesema kuwa wameamua kuwaleta waendesha bodaboda kwenye ziara hiyo ili waweze kujionea mambo mazuri yanayofanywa na Serikali ya awamu ya tano ili wakawe mabalozi wazuri kwa wenzao.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Kagera, Brigedia Jeneral Marco Gaguti ameipongeza Serikali kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya Katika utekelezaji wa miradi yenye lengo la kutatua kero kwa wananchi.
Aidha Brigedia Jenerali Gaguti amesema mbali na ziara hiyo Jpia walifanya mashindano ya mpira wa miguu kati ya timu ya bodaboda Mtwara na timu ya bodaboda Kagera kwa lengo kujenga uzalendo kwa kundi hilo la vijana na kuwafanya kuwa mabalozi wazuri wa shughuli za Serikali.





