Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge
Akizungumza Katika ziara hiyo RC Kunenge ameonyesha kuridhishwa na namna kiwanda hicho kinazalisha nyama kwa viwango vya kimataifa jambo linalopelekea 80% ya nyama inayozalishwa Kiwandani hapo kuuzwa nje ya nchi.
Aidha RC Kunenge amepongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kutafsiri kwa Vitendo ndoto ya Rais Dkt. John Magufuli ya Tanzania ya Viwanda jambo lililowezesha kutoa ajira na kuchangia ukuaji wa uchumi.
Hata hivyo RC Kunenge amesema kiwanda hicho pia kitasaidia wafugaji kutoka mikoa mbalimbali nchini kupata soko la uhakika la kuuza mifugo yao kwa Bei yenye tija.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho Bw. Rashid Abdilah amesema kwa Sasa kiasi kikubwa Cha nyama nayozalisha wanaiuza kwenye mataifa ya Falme za kiarabu Kama Oman, Quatar na Kuwait na kueleza kuwa mahitaji ya nyama nje ya nchi bado ni makubwa.

