Mgeni Rasmi wa mashindano ya NBC Dodoma Marathon ambaye ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mama Samia Suluhu Hassan akitoa hotuba yake wakati wa kuhitimisha mashindano hayo.
Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi.
Mama Samia amesema hayo wakati akiongea na wanamichezo walioshiriki mbio za Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Dodoma Marathon yaliyofanyika leo Novemba 22, 2020 Jijini Dodoma, ambapo katika mashindano hayo, amewapongeza wanawake kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mbio hizo hatua inayoonesha ni mwanzo mzuri wa kupambana na saratani ya shingo ya kizazi nchini.
“Akinamama mjitokeze kupima afya zenu mapema, msiogope kwenda kupima saratani ya mlango wa kizazi hatua inayosaidia kupambana na saratani hii na kulinda afya za watu wetu” amesema Mama Samia.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Theobald Sabi amesema kuwa benki hiyo wameona ni vema mapato yote yanayotokana na usajili wa wanariadha zielekezwe kwenye vita na mapambano dhidi ya ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Bishara (NBC) Bw. Theobald Sabi akizungumza
wakati wa hafla ya kuhitimishwa kwa mbio za NBC Dodoma Marathon.
Sabi ameongeza kuwa njia zote zinazotumika kwenye mbio za NBC Dodoma marathon zimepimwa na mtaalamu kutoka Shirikisho la Riadha Duniani Oktoba 17, 2020 na kutunukiwa vyeti vya utambuzi na uthibitisho na vipo tayari Dodoma.
Mbio hizo za NBC Marathon zimehusisha wanariadha 3000 wakijumuisha wanariadha kutoka hapa nchini, 19 kutoka nchini Kenya, 12 kutoka Uganda pamoja na wanariadha wanne (04) kutoka Malawi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan
akishiriki mbio za NBC Dodoma Marathon zilizofanyika leo Novemba 22, 2020 Jijini Dodoma.