
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge.
RC Kunenge amesema hayo wakati wa ufunguzi wa wiki ya kitaifa ya kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza iliyoanza Novembea 07-14 mwaka huu, kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo amesema katika wiki hiyo wananchi watapata fursa ya kupima magonjwa mbalimbali bure na kupatiwa ushauri wa kitaalamu.
Aidha RC Kunenge amesema kwa kuwa magonjwa hayo yanaweza kuzuilika ni vyema wananchi wakaanza kuchukua tahadhari mapema kwa kuhakikisha wanazingatia ulaji bora, kupunguza ulevi usiofaa, kupunguza uvutaji wa sigara na kuzingatia michezo.
Pamoja na hayo RC Kunenge amesema kuwa kwa upande wa serikali itaendelea kutoa elimu ya kutosha ya namna bora ya kukabiliana na magonjwa hayo na kuendelea kuboresha na kuongeza miundombinu mbalimbali ya afya