
Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa,
Akizungumza katika uzinduzi wa kituo hicho, Mkuu wa wilaya ya Morogoro Bakari Msulwa, amesema kuwa kukamilika kwa kituo hicho kunaendelea kuongeza sifa ya Manispaa ya Morogoro kufikia hadhi ya kuwa Jiji na kuwaomba wananchi kutunza miundombinu ya stendi hiyo ili iweze kuwanufaisha kwa muda mrefu zaidi.
Mhandisi Mnene James, ambaye ni Meneja wa TARULA wa Manispaa ya Morogoro, ndiye aliyepewa jukumu la kusimamia mradi huo, ambapo amesema kuwa kituo hicho cha mabasi kina uwezo wa kuchukua magari zaidi ya 50 kwa wakati mmoja huku ikitarajiwa zaidi ya shilingi Milioni 3 kukusanywa kila mwezi, sambamba na kuongeza fursa kwa wafanyabiashara wadogo.