
Kulia ni Katibu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya
Bw. Kusaya ameyasema hayo jijini Dodoma alipokuwa na ziara ya kikazi katika ofisi za Tume ya Taifa ya Umwagiliaji,ambapo amesema Serikali ina mpango wa kuboresha mundombinu yote chakavu katika sekta ya umwagiliaji na kufufua skimu za zamani na kuongeza skimu mpya
Pia amesema Serikali pia imeona umuhimu wakuongeza wataalamu wa sekta hiyo katika ngazi za wilaya na itafikia ngazi ya kata na kijiji ili kuweza kumfikia mkulima kwani kilimo cha umwagiliaji ndicho kilimo cha uhakika na mkombozi kwa mkulima.
“Wakulima watapata huduma za uhakika zaidi na kunufaika na kilimo cha umwagiliaji” amesema Kusaya
Aidha katibu Kusaya, alikagua mitambo iliyopo katika ofisi za Tume hiyo inayotumika kujengea na kuboresha miuondombinu ya umwagiliaji.