Tuesday , 27th Oct , 2020

Eden hazard amerejea Real Madrid na ni sehemu ya kikosi kitakacho cheza mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Borussia Monchengladbach leo usiku.

Eden Hazard hajacheza mchezo hata mmoja msimu huu wa 2020-21

Hazard hajacheza mchezo hata mmoja msimu huu 2020-21 na mara ya mwisho kuitumikia Los Blancos ilikuwa Agosti 7 kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Manchester City ambazo ni siku 81 zilizopita.

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane anasema kila mchezaji aliyesafiri na timu yupo tayari kwa mchezo.

Kuhusu Hazard Zidane alisema "Ikiwa Hazard yuko nasi ni kwa sababu yuko vizuri na hiyo ni habari njema. Sisi sote tunafurahi kumwona yuko pamoja nasi.”

Usajili wa Hazard ndani ya Real Madrid bado haujalipa kama ilivyotegemewa na wengi.

Mshambuliaji huyo alijiunga na Real Madrid akitokea Chelsea kwa ada ya uhamisho ya pauni milion 104 ambazo ni zaidi ya bilioni 314 kwa pesa za kitanzania lakini kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara alicheza michezo 22 na akafunga goli 1 kwenye mashindano yote.

Mchezo wa kwanza wa kundi B Madrid walifungwa na Shakhtar Donetsk 3-2 wiki iliyopita hivyo kurejea kwa Hazrd kutampa kocha Zidane uwanda mpana wa kuchagua wachezaji katika safu ya ushambuliaji.

Mchezo mwingine wa kundi hilo Shakhtar Donetsk wataminyana na Inter Milan .

Ratiba ya michezo mingine ligi ya mabingwa ulaya ni.

Kundi A

Lokomotiv Moscow Vs Bayern Munich

Atletico Madrid Vs RB Salzburg

Kundi C

FC Porto Vs Olympiacos

Marseille Vs Manchester City

Kundi D

Atalanta Vs Ajax

Liverpool Vs FC Midtylland