
picha ya soko la Tabata Muslim
Wakizungumza na kurasa hii leo wamesema soko hilo ni la muda mrefu licha ya kuwa ni soko kubwa lakini haliboreshwi na halmashauri imekua hailizingatii na kudai kuwa baadhi ya maeneo katika soko hilo yamerekebishwa na fedha zao pamoja misaada ya watu wengine.
Aidha Wafanyabiashara hao wamesema kuwa changamoto nyingine ni pamoja na maeneo lilipo soko hilo ambalo lipo nyuma ya kituo cha mafuta hivyo wakati mwingine kukosa wateja kutokana na kuwepo katika eneo lililojificha.