Tuesday , 13th Oct , 2020

Mgombea Ubunge jimbo la Kawe kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Halima Mdee, amesema kuwa hajakubaliana na maamuzi ya Kamati ya Maadili ambayo yamemsimamisha kutofanya kampeni siku 7 na anaelekea Tume kuwasilisha rufaa yake.

Mgombea Ubunge jimbo la Kawe kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Halima Mdee

Mdee ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa Kamati ya Maadili ilitoa hukumu bila kumsikiliza wala kusikiliza ushahidi wake aliowasilisha.

“Kwa mujibu wa tuhuma nilizopewa na Chama cha Mapinduzi kuwa namchonganisha Gwajima na madhehebu mengine na waumini wake, nimewasilisha ushahidi mbele ya Kamati ya Maadili lakini hawajataka kunisikiliza”, amesema Mdee.

Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CHADEMA, Halima Mdee amefungiwa kufanya Kampeni kwa siku saba kuanzia Oktoba 12 hadi Octoba 18 kwa madai ya kukiuka maadili ya uchaguzi.