Sunday , 11th Oct , 2020

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Ali Makame Issa, Zanzibar, amesema tayari chama hicho kimeshakata rufaa baada ya kuzuiwa kutokufanya kampeni katika jimbo la Mtwara mjini kwa muda wa siku kumi.

Wanachama wa CUF

Akizungumza na EATV Digital, amesema kuwa zimeshatimia siku tatu tangu kuzuiwa kwao kufanya shughuli za kampeni katika jimbo hilo baada ya malalamiko yaliyopelekwa katika Kamati ya Maadili ya Tume ya Uchaguzi juu ya ukiukwaji wa maadili ya uchaguzi .

 "Chama kimekata rufaa pamoja na adhabu iliyopewa na malalamiko yao wanataka ile adhabau ipunguzwe pia kwasababu siku kumi ni siku nyingi sana ikiwa ni mgombea unafanya kampeni ukaambiwa ukae tu" alisema  Ali Makame Issa

Aidha Makame ameweka wazi imani waliyonayo juu ya  mgombea wa chama chao katika jimbo hilo Bw. Maftah Abdallah Nachuma ambaye anatetea nafasi yake yakuendelea kuliwakilisha jimbo kuwa ni mgombea anayesubiria kuapishwa.

Hata hivyo  Makame amesema kuwa wanaamini kuwa kampeni walizozuwia kufanya ni kwa upande wa Ubunge hivyo katika ngazi nyingine kampeni bado zinaendelea.