
Wafanyakazi wa Tigo wakiwa maeneo ya Kawe
Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja wa Tigo Mwangaza Matotola, amesema zoezi hilo walilolifanya leo pia limefanyika nchi nzima kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa kuwatembelea wateja wao mitaani na kuwapa huduma za mtandao huo.
“Kwa upande wa mkoa wa Dar es salaam wafanyakazi wa Tigo watakwenda maeneo mbali mbali na kukutana na wateja na kuzungumza nao na kujua changamoto wanazokutana nazo ili kuzitatua” amesema Matotola
Amesema kampuni ya Tigo imeongeza ufanisi mkubwa katika utoaji wa huduma zake kwa kuzingatia mahitaji ya wateja na kwamba watahakikisha mteja wa Tigo mwenye changamoto za aina yoyote zinatatuliwa papo hapo.