Tuesday , 22nd Sep , 2020

Chama cha siasa cha upinzani cha ACT-Wazalendo kupitia Mwanasheria wa chama hicho kimedai kuwa kiu ya Watanzania ni kuona vyama vya upinzani vikiungana katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu

Pichani ni Mwanasheria wa chama hicho Omary Shaban

Akizungumza na wanahabari Mwanasheria wa chama hicho, Omary Shaban amesema kuwa suala la Mwenyekiti wa chama hicho Taifa kutangaza kumuunga mkono mgombea wa urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu litaongelewa muda sio mrefu na mamlaka zinazohusika.

Akizungumzia rufaa za wagombea wao wa ubunge Omary amedai kwamba wagombea wao walijaza fomu hizo kwa umakini na hakukuwa na mapungufu kama ambavyo tume iliainisha.

Hapo Jana Menyekiti wa ACT-Wazalendo Taifa Maalim Seif Sharif Hamad alizungumzia kumuunga mkono mgombea urais wa Chadema Tundu Lissu.