
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Chadema, Reginald Munisi akizungumza na waandishi wa habari (hawapopichani).
Uamuzi huo unalengo la kutoa nafasi ili waweze kuendelea na kampeni za uchaguzi kwa kuwa sasa wanashindwa kufanya hivyo kutokana kutokuwa na maelezo yoyote ya maamuzi ya rufaa hizo.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Chadema, Reginald Munisi, ametoa ombi hilo leo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari huku akiwa na wagombea hao waliokatiwa rufaa na kusema kuwa tume haijaainisha wazi wagombea ambao rufaa zao zimekataliwa kwa kuwa hadi sasa hawajapata barua yoyote ya kuonyesha kama rufaa zao zimekubaliwa au zimekataliwa.
Kwa upande wao wagombea wa nafasi hizo waliokatiwa rufaa wamesema kwa sasa wanashindwa kufanya shughuli zao za kisiasa hasa ikizingatiwa kwamba kampeni zinaendelea katika maeneo yao jambo ambalo linawafanya kushindwa kujinadi kwa wananchi.