
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu na Kaimu Mkurugenzi wa Lojistiki, Byekwaso Tabura.
Hayo yameelezwa leo Septemba 21, 2020 na upande wa mashitaka wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutwaja.
Mbele ya Hakimu Mkuu, Richard Kabate, wakili wa Takukuru, Moza Kasubi amedai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa. Hakimu Kabate baada ya kusikiliza hoja hizo ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 5, 2020 itakapotajwa tena.
Miongoni mwa mashitaka yanayowakabili washitakiwa ni kati ya tarehe 1 Julai, 2016 na 30 June, 2019 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, kwa makusudi washtakiwa waliongoza genge la uhalifu.
Shitaka la pili ni kuisababishia hasara MSD, tukio wanalodaiwa kulitenda kati ya Julai mosi, 2016 na tarehe 30 June, 2019, katika eneo la MSD lililopo Keko, washtakiwa waliisababishia MSD hasara ya shilingi bilioni 3.8.
Pia, Bwanakunu, anadaiwa kati ya tarehe 1 Julai, 2016 na 30 Juni, 2019 katika Ofisi za MSD zilizopo Keko, kwa makusudi alikiuka sheria ya umma kwa kutumia madaraka yake vibaya kwa kuwaongezea nyongeza ya mishahara na posho wafanyakazi wa MSD, bila kibali cha Katibu Mkuu Utumishi na hivyo kuisababishia hasara Mamlaka hiyo kiasi cha shilingi bilioni 3.
Shitaka la nne ni kuisababishia hasara ya shilingi 85 milioni mamlaka, shtaka linalowakabili washtakiwa wote, huku katika shtaka lingine wakituhumiwa kutakatisha fedha kiasi cha shilingi bilioni 1.6.