Monday , 21st Sep , 2020

Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amewaahidi wanachi wa Ngara  kuwa mfariji wao na kuwatendea haki kwani anafahamu maana ya kufarijiwa.

Mgombea Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu.

Lissu ametoa ahadi hiyo leo septemba 21, wakati akizungumza na wananchi wa Ngara  ambapo amesema kutokana na misaada aliyopata kipindi cha matibabu yake anafahamu maana halisi yakuwa mfariji kwa watu.

"Ninafahamu maana yakutokutendewa haki hivyo nitawatendeeni haki, nafahamu maana yakufarijiwa unapokuwa na shida kwa sasbabu nimepata faraja kubwa nimetibiwa kwa misaada yenu kwa hiyo nitakua mfariji wenu” amesema Tundu Lissu.

Tundu Lissu ameongeza "Kwenye uchaguzi mkuu huu ni fursa yetu,tupate rais anayefahamu kwamba wajibu wa kwanza wa rais ni kuwa mfariji mkuu watu wanapopata shida, panapokuwa na kilio unaenda kuhani kilio penye shida unenda kutoa faraja sio unapeleka kejeli”.

Lissu leo anafanya kampeni zake katika mkoa ya Geita na Kagera.