Saturday , 29th Aug , 2020

Klabu ya soka ya Yanga ambayo ndiyo mabingwa wa kihistoria wa Ligi kuu ya Tanzania Bara ,imejinasibu kuwa na kikosi kipana na chenye thamani kubwa ya Bilioni mbili na nusu za Kitanzania.

Nyota wapya wa Yanga, Carlinhos (Kushoto) na Tuisila Kisinda)Kulia) wakiwa mazoezini kwenye uwanja wa Chuo cha Sheria Jijini Dar es salaam.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu hiyo , Hassan Bumbuli wakati akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya maandalizi ya klabu yao kuelekea kilele cha wiki ya Mwananchi.

Bumbuli amesema mashabiki na wanachama wa Yanga wanapaswa kujitokeza kwa wingi kesho katika Uwanja wa Mkapa uliopo Jijini Dar es salaam wakiwa kifua mbele kuja kuwashuhudia wachezaji wao wapya wenye viwango vya juu na thamani watakobeba matumaini yao katika msimu unaokuja.

Miongoni mwa sajili zilizotikisa ni pamoja wa Carlinhos,Tuisila Kisinda, Tonombe Mukoko hao ni kwa wakigeni lakini kwa wazawa ni pamoja na mlinzi Bakari Mwamnyeto na hata Farid Mussa aliyemaliza mkataba wake na Tenerife ya Hispania.