
Nahodha wa Barcelona Lionel Messi akiwa na huzuni baada ya Klabu yao kutupwa nje ya michuano ya Ulaya.
Nahodha wa zamani wa Barcelona Carlos Puyol amemuunga mkono Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi juu ya uamuzi wake wa kutaka kuondoka katika Klabu hiyo.
Puyol ameandika kuwa kupitia ukurasa wake wa Twitter ''Respect& Admiration, Leo.You have all my support,friend''(Heshima na pongezi,Leo.Ninakuunga mkono rafiki yangu'').
Tweet hiyo ikajibiwa na mshambuliaji Luis Suarez ambaye ameonyeshwa mlango wa kuondoka klabuni humo.