
Mchezo wa UEFA Super Cup kati ya Bayern Munich dhidi ya Sevilla utachezwa katika uwanja wa Pukas mjini Budapest nchini Hungary
Shirikisho la soka barani ulaya UEFA limethibitisha kuwa mashabiki wataruhusiwa kuingia uwanjani kushuhudia mchezo utakao wakutanisha mabingwa wa klabu Bingwa ulaya UEFA Bayern Munich ya Ujerumani dhidi ya mabingwa wa michuano ya UEFA Europa League Sevilla ya Hispania.
Ni asilimia 30% tu ya mashabiki ndio watakao ruhusiwa kuingia uwanja kulingana na ukubwa wa uwanja unachukua mashabiki wangapi, kwa mujibu wa UEFA uwanja huo unachuka mashabiki 680000 hivyo kwa wastani ni mashabiki 20,000 ndio watakao ruhusiwa kushuhudia mchezo huo wakiwa uwanjani.
Rais wa shirikisho la soka barani ulaya Aleksander Ceferin amesema ni muhimu kuonyesha kuwa mpira wa miguu unaweza kuhimili vipindi vigumu, na bila mashabiki mchezo huo unapoteza thamani yake.
Ceferini amesisitiza kuwa wanataka kuutumia mchezo wa Super CUP kama kipimo ilikufanya tathimini kama kunauwezekano wa mashabiki kurejea tena viwanjani hivi karibuni.
Mashabiki wamekuwa hawaruhiswi kuingia viwajani toka ligi mbali mbali kurejea kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona.
Bayern Munich wamefanikiwa kufuzu kucheza mchezo wa Super CUP baada ya kuifunga PSG bao 1-0 katika mchezo wa fainali ya klabu bingwa na ushindi wa mabao 3-2 ulitosha kuipa Sevilla ubingwa wa Europa League dhidi ya Inter Milan. Na kukata tiketi ya kucheza katika mchezo wa Super CUP.