
Prof. Mohamed Janabi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo(JKCI)
Akizungumzia kampeni ya kurejesha tabasamu ambayo imekuwa ikifanywa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi amesema wamekuwa wakishirikiana na wadau mbalimbali ili kuchangia gharama kwa watoto wenye ugonjwa moyo ili kuokoa maisha yao.
"Serikali imewekeza kiasi kikubwa kwenye sekta ya afya lakini jamii haina budi kujitokeza katika kuchangia gharama za matibabu kutokana na ongezeko la mahitaji kwenye jamii", amesema Profesa Janabi.
Aidha, amewataka Watanzania kuwa na utaratibu wa kupima afya zao mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi, huku akiwaasa wadau wa makampuni kuzidi kujitokeza kuchangia gharama za matibabu huku akiishukuru Serikali kwa uwekezaji mkubwa ilioufanya kwa wataalam na vifaa.
"Ukiwa na utaratibu wakujua hali yako yua kiafya inakusaidia kupanga bajeti katika afya na kurahisisha utekelezaji wa majukumu mengine katika jamii, suala la magonjwa yasiyoambukiza limekuwa changamoto miongoni mwa jamii hii zaidi huchangiwa na ukosefu wa elimu" ameongeza.