Thursday , 6th Aug , 2020

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jaffo, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za utoaji wa tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)msimu wa 2019/2020, zinazotarajiwa kufanyika kesho jioni katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jaffo katika moja ya majukumu yake ya Kitaifa.

Tuzo 18 zinatarajiwa kutolewa siku hiyozikiwemo tuzo tatu mpyaambazo ni Tuzo ya Beki Bora, Tuzo ya Kiungo Bora na Tuzo ya Seti Bora ya Waamuzi.

Tuzo ya Seti Bora ya Waamuzi itahusisha Mwamuzi wa Kati, Mwamuzi Msaidizi Namba Moja, Mwamuzi Msaidizi namba mbili na Mwamuzi wa Akiba ambao wote watazawadiwa.

Pia zipo tuzo nyingine zitakazotolewa siku hiyo ambazo baadhi ni za kikanuni na tayari washindi wake wameshajulikanakamaBingwa(SimbaSC), Mshindi wa pili(YangaSC), Mshindi wa tatu(AzamFC), Mshindi wa nne(NamungoFC) na Mfungaji bora (Meddie Kagere).

Shughuli kubwa kesho ni Tuzo ya Mchezaji bora wa VPL inayowaniwa na mabeki Nicolas Wadada (Azam FC), Bakari Mwamnyeto (Coastal Union FC) na kiungo Cletous Chama (Simba SC), ambapo tuzo nyingine ni Kocha Bora inayowaniwa na Sven Vandenbroeck (Simba SC), Hitimana Thiery(Namungo FC)na Aristica Cioaba (Azam FC)wakati Beki Bora ni Bakari Mwamnyeto (Coastal Union FC), David Luhende (Kagera Sugar FC) na Nico Wadada (Azam FC).

Tuzo ya Kiungo Bora inawaniwa na Lucas Kikoti (Namungo FC), Cletous Chama (Simba SC)naMapinduzi Balama (Yanga). Wanaowania tuzo ya GoliBora ni Sadallah Lipangile ((KMC) vs Mtibwa), Luis Miquissone ((Simba) vs Alliance)na Patson Shikala ((Mbeya City) vs JKT Tanzania).