Akizungumza na East Africa Radio, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wavu Mkoa wa Dar es salaam DAREVA, Siraju Mwasha amesema licha ya kualika vilabu kutoka nchi za Kenya wamealika pia vilabu kutoka nchi za Uganda na Rwanda lakini mpaka sasa bado vilabu hivyo bado havijahakiki ushiriki wao na wanatarajia kupata majibu juu ya ushiriki wao ifikapo Jumatatu.
Mwasha amesema katika mashindano hayo wameamua kushirikisha vilabu kutoka nje ya nchi kutokana na hadhi ya mashindano hayo ambayo ni ya kitaifa na pia ushirikiano walionao baina ya nchi hizo katika mchezo huo.