Wednesday , 29th Jul , 2020

Mabingwa wa kihistoria wa michuano ya mpira wa kikapu ya Sprite Bball Kings yanayoandaliwa na kituo cha EATV LTD, Mchenga Bball Stars wataanza kampeni zao za kucheza ligi ya Taifa ambapo siku ya Jumamosi watachuana na Jogoo katika mchezo wa D League katika uwanja wa Harbours Club uliopo Ba

Baraka Sadick (Kati kati pichani) ambaye ndiye MVP kwa misimu miwili mfululizo ya Sprite BBall Kings akishangilia ushindi na wenzake.

Muasisi wa timu hiyo Mohamed Yusuph alizungumza na kipindi cha Michezo cha KIPENGA kinachoruka kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa saa 2 usiku, East Africa Radio ambapo amesema ili kuonyesha thamani ya michuano ya Sprite Bball Kings ambayo ndio iliyowatoa, hawana budi kupeleka ushindani katika ligi hadi kimataifa.

Katika hatua nyingine Yusuph ambaye pia ni kocha, amesema malengo makubwa zaidi ni kuhakikisha wanawaendeleza vijana kielimu kwa kuwa wamedhamiria kuwatengeneza njia za kupata ajira katika taasisi mbali mbali zikiwemo za majeshi.

Hivyo wataendelea kuviendeleza vipaji na kupitia nafasi hizo wanawasaidia wazazi kuchangia ada kwa watoto wao ambao wanataka kufika mbali, kielemu lakini pia kwa sasa hata Jeshi limekua likifuatilia vijana wao hivyo ni fursa kubwa kwao kutimiza ndoto kubwa.

Mchenga ilitwaa ubinbwa wa Sprite Bball Kings kwa misimu mitatu mfululizo na kujizolea kitita cha shilingi milioni 10 katika kila msimu huku ikitoa MVP katika kila msimu.